Jifunze Kuongeza Speed & Performance ya Computer yako.




Karibu sana mpenzi msomaji, ni siku nyingine tena tunakutana, kwa siku ya leo tunakwenda kujifunza hatua tatu ambazo unaweza ukazifanya kwenye computer yako ili kuifanya computer yako iwe na performance inayotakiwa, kuyafahamu yote haya basi ongozana nami katika hatua zifuatazo:-


Hatua ya kwanza
·        Bonyeza start button

·        Andika neno “RUN” kwenye search box na Bonyeza kitufe cha “enter

·        Andika neno “%temp%” likiwa na alama ya asilimia kila upande, kama inavyoonekana kwenye picha hapo chini na Bonyeza kitufe cha “enter” au “Ok

·        Chagua file zote ambazo zimeonekana hapo kwa kubonyeza kitufe cha “crtl” pamoja na “A” kwa pamoja (crtl+A).


·        Delete files hizo ulizozichagua.

·        Weka alama ya tiki na Bonyeza option ya “skip

Hatua ya Pili
·        Bonyeza start button

·        Andika neno “RUN” kwenye search box na Bonyeza kitufe cha “enter


·        Andika neno “prefetch” kama inavyoonekana kwenye picha hapo chini na Bonyeza kitufe cha “enter” au “Ok”.

·        Bonyeza kitufe cha “enter” au “Continue” ili kuendelea hatua inayofuata.


·        Chagua file zote ambazo zimeonekana hapo kwa kubonyeza kitufe cha “crtl” pamoja na “A” kwa pamoja (crtl+A).

·        Delete files hizo ulizozichagua.

Hatua ya Tatu
·        Bonyeza start button

·        Andika neno “Disk cleanup” kwenye search box na Bonyeza kitufe cha “enter”

·        Bonyeza kitufe cha ‘enter” au “Ok” ili kuendelea.

·        Mwisho kabisa, weka alama ya tiki sehemu zote kama inavyoonekana hapo kwenye picha hapo chini na Bonyeza kitufe cha “enter” au “Ok”.


Mpaka hapo ni matumaini yangu utakuwa umejifunza  na ahsante kwa kuwa nasi, kama una maoni, mapendekezo pamoja na ushauri usisite kutuandikia  hapo chini kwenye sehemu ya comment


Kwa kujifunza zaidi tafadhali download hapo chini
2.86 MB


Kwa maoni, ushauri, mapendekezo au msaada kuhusu chapisho hili, usisite kutuandikia hapo chini katika kisanduku cha maoni nasi tutayafanyia kazi.

Post a Comment

[facebook][blogger]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget